Abdallah Kibadeni kuendelea kuinoa Ruvu JKT


Klabu ya JKT Ruvu imempa fungu la usajili Kibadeni ambaye awali alisema wazi kuwa baada ya msimu ataachana na klabu hiyo
Kocha Mkuu wa timu ya JKT Ruvu Abdallah Kibadeni ameamua kubaki kuendelea kukinoa kikosi cha timu hiyo msimu ujao baada ya uongozi wa timu hiyo kumpa fungu la usajili.
Kibadeni ameiambia Goal, amefuraishwa na mikakati ya uongozi wa timu hiyo ambayo inalengo zuri la kuiona timu hiyo ikifanya vizuri msimu ujao na hilo linawezekana kutokana na kiasi cha pesa alichopewa kwa ajili ya kufanya usajili.
“Nitabaki kwa sababu ya mapingo mizuri iliyopo msimu ujao nataka kuisuka upya JKT Ruvu, na kuifanya kuwa timu ya ushindani kama ilivyokuwa siku za nyuma hakuna linaloshindikana wachezaji wapo wengi sina shaka kwamba msimu ujao tutakuwa bora zaidi ya msimu uliopita,” amesema Kibadeni.
Ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba katika mchezo wa mwisho wa ligi ya Vodacom msimu uliopita ndiyo ulioikoa timu hiyo isiweze kushuka daraja na sasa Kibadeni atakuwa na kazi ya kuisuka upya timu hiyo ili msimu ujao isiwe ya kusuasua kama ilivyokuwa msimu uliopita.
-By Zuber Karim Jumaa
Previous
Next Post »