MWANAMAMA kutoka katika kiwanda cha filamu Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amewatemea cheche wanaomsengenya kuwa amekimbiwa na mumewe hivyo kuwataka wamuache kwani hawezi kuachwa kamwe.
Akizungumza na GPL, Cathy alisema tangu mumewe ahamie kikazi Zanzibar maneno yamekuwa mengi sana kutoka kwa watu wake wa karibu kwamba ameachwa kitu ambacho siyo kweli kwani wako vizuri na mambo yao ya kifamilia yanakwenda vizuri.
“Nawashangaa sana wanaonisengenya kwamba nimeachwa, jamani siwezi kuachwa na mume wangu kamwe ila tumekuwa mbali kwa sababu tu ya kazi maana alihamishiwa Zanzibar na mimi nikabaki huku Dar ili kuendeleza miradi yetu mingine maana tungehamia wote huko tungepoteza vitu vyetu vingi vya maendeleo,” alisema Cathy bila kuwataja majina ‘wabaya’ wake.
Chanzo: GPL
ConversionConversion EmoticonEmoticon