Ifahamu Swahili Hip hop Band iliyopania kuipeleka hip hop ya Tanzania kwa ‘live band’


“Tulianzisha bendi ya hip hop baada ya kukubali mchango wa wakongwe wa sanaa hii katika mambo waliyoyafanya,” member wa bendi hiyo, Troubadour ameniambia.
“Kwahiyo sisi tukafikiria njia za kuweza kuusogeza muziki na utamaduni wetu mbele zaidi kwa njia tofauti. Njia hii ya muziki wa hip hop wenye vionjo vya asili unaofanywa kwa maonesho ya moja kwa moja tulioupa jina la Tubite Fleva,” ameongeza,
Hadi sasa bendi hiyo ina watu sita, wanaume watatu na wanawake watatu.
“Tunategemea kuongeza watu wa kucheza pamoja na wapiga vyombo,” anasema.
“Bendi yetu ina miaka mitatu imeanza mwaka 2014 na matumbuizo tunayafanya kwenye maonesho ya wazi na maeneo mengine tutakapohitajika.”
“Tofauti ya muziki wetu na hip hop nyingi ni mahadhi pamoja na maudhui ya wahusika ikiwa tumebeba asili ya muafrika na tamaduni zake,” amesisitiza rapper huyo.
“Katika kufanya live bendi ya hip hop kuna faida kwa sababu unaweza kuwasilisha ujumbe zaidi kulingana na mazingira.” Anasema hadi sasa wameshatoa wimbo mmoja redioni uitwao Africa Tubite pamoja na video yake.
Kuna changamoto za hapa na pale wanazokabiliana nazo.
“Changamoto kubwa tunayokumbana nayo ni vifaa kama drums, guitar, vinanda, vipaza sauti na speaker zinazokidhi tunachokifanya. Na hii ni kwa sababu muziki wetu unahitaji uwekezaji mkubwa kwa sasa.”
“Mipango ya baadaye ni kuwa na kampuni kubwa inayohusika na mambo ya asili ya mwafrika itakayojihusisha na utengenezaji wa nguo zenye brand zetu za kiafrika,na promotion ya mali asili hususani vivutio vya utalii,” amesema Troubadour.
“Tunakaribisha uwekezaji kwa sasa kwenye bendi yetu.”


Ameongeza pia kuwa wiki hii wanaachia kazi mpya.
Previous
Next Post »