Mama yake Wema Sepetu, Mariam Sepetu amefunguka na kueleza jinsi anavyoumizwa na stori za uongo kuhusu mwanae ambazo zimekuwa zikiandikwa katika magazeti ya udaku.
Akizungumza katika kipindi cha Clouds E cha Clouds TV Alhamisi hii, Bi Mariam amesema amekuwa akigombana mara kadhaa na baadhi na viongozi wa magazeti ya udaku kuhusu stori za uongo.
“Naumia sana kama mzazi, Wema alishaambiwa kwamba ana maradhi ya ngono, kama mzazi najisikia vibaya sana,” alisema Mama Wema. “Mimi nikishasikia hivyo nawafuata watu wa magazeti, nagombana nao sana. Kuna wakati nampigia Wema namuuliza jana ulitoka, anasema hajatoka, ukiwa kama mzazi inauma sana, wao wanauza magazeti kutokana na stori za uongo za mwanangu,”
Aliongeza, “Nimeshapigana na watu kuhusu Wema, wanakuja nyumbani wanaanza kuongea maneno maneno ambayo hayaeleweki,”
-by Bongo5
ConversionConversion EmoticonEmoticon