Nipo tayari kuigiza nimekufa Hollywood lakini siyo kuwa punga – Idris Sultan




Mshindi wa shindano la Big Brother 2014, Idris Sultan amefunguka na kuzungumzia mpango wa kuingia rasmi kwenye tasnia ya ugizaji

Akiongea na Bongo5 hivi karibuni, Idris amesema mpango wake mkubwa ni kwenda kuigiza Hollywood na siyo hapa nyumbani.

“Nia yangu ni kuingia kwenye tasnia ya filamu,” alieleza Idris Sultan baada ya kuulizwa kama ana mpango wa kuingia kwenye tasnia ya filamu.

“Target yangu kubwa ni Hollywood, yaani hata nikiambiwa niende sasa hivi nikaigize nimekufa nitaenda fasta ila kasoro kwenda kuigiza kuwa punga Hollywood, hiyo hapana,” aliongeza.

Katika hatua nyingine, Idris amesema tayari ameshasaini madili ya kuwa balozi wa makampuni kadhaa na baada ya mwezi wa ramadhani atayaweka wazi.

-Source Bongo5
Previous
Next Post »