UEFA inajipanga kutoa adhabu kwa Urusi


Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, kufuatia vurugu za mashabiki wa Urusi zilizotokea katika mchezo wa Euro 2016 kati ya England dhidi ya timu ya taifa ya Urusi, limekaa na kuanza kujadili namna ya kuidhabu Urusi kutokana na vitendo hivyo.


UEFA inaijadili Urusi kutokana na mashabiki wake kuwafanyia fujo, kuwapiga na kuwafanyia vitendo vya kibaguzi mashabiki wa timu ya taifa ya England katika mchezo uliochezwa jana June 11 2016 katika mji wa Marseille na kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Kwa mujibu wa shuhuda anaeleza vurugu hizo zilizoendelea hadi nje ya uwanja, zilianzia ndani ya uwanja wakati ambao mechi ilikuwa ikikaribia kumalizika baada ya shabiki waUrusi kurusha miale ya moto kwa mashabiki wa England, kufutia tukio hilo UEFAinatarajiwa kutoa adhabu kali kwa Urusi.

-By 
Previous
Next Post »