Kwa watumiaji wa vilevi hii ni bahari njema kwenu, hakuna mtu anaependa starehe iliyo na mateso baadae, kwanini uwaze dawa ya kutibu maumivu ya pombe za jana wakati kuna uwezo wa kuzuia maumivu hayo, hangover inatesa sana na wapo watu wanaotumia maji mengi kesho yake, wapo wanaokunywa vinywaji vya baridi sana au kunywa tena pombe wanaita kuzimua, hii yote ikiwa ni njia ya kutoa hangover,
Ila kuna mbinu ambazo ukizitumia zitakufanya ustarehe na unywe pombe bila mawazo ya kuamka na hangover Asubuhi inayofata.
1.JUA KIWANGO CHAKO CHA MWISHO.
Kila mtu hujua kiwango chake, kuna wakati unapopata pombe au “Masanga” kama inavyoitwa mitaani,inafikia wakati unahisi kabisa mambo yanaanza kuwa sio mambo hasa pale unapojiona sasa unalewa hali ambayo kila mtu hujua,wengine bia 3,7,10 na wengine wanaweza maliza kreti, kila mtu na staili yake, ila jambo la kukusaidia usiwe na hangover kesho yake ni kuacha kunywa pale tu unapojua umefikia kikomo.
2.EPUKA POMBE ZILIZO NA SUKARI.
Kuna pombe zinatajwa kuwa na sukari nyingi kuliko kawaida,hivyo zitakufanya unywe sana na kwa haraka sana na hata kulewa pia na si ajabu ukajikuta umekunywa pombe nyingi kuliko kawaida. Hii itakusumbua kwani ukilewa sana unajua nini utakipata siku inayofata.
3.USIKAE MBALI NA VINYWAJI VISIVYO NA KILEVI.
Kunywa maji mengi ukiwa umepata pombe kwa mda mrefu, hii itasaidia kupungua kasi ya kilevi ulichokunywa, kaa karibu na aina nyingine ya kinywaji ambacho hakina kilevi kabisa.
4.KULA CHAKULA.
Tuache zile tabia za kupania pombe za bure au za sherehe, wakati mlo wako mawazo, kama unajua unaenda kunywa pombe hakikisha unakula chakula cha kutosha na unashiba,hii itakusaidia sana.
5.KUNYWA POMBE ISIYO NA MCHANGANYIKO WOWOTE.
Kuna baadhi ya pombe kali na zina mchanganyiko wa viungo tofauti tofauti ambavyo husababisha hangover, kwahiyo kuwa makini katika uchaguaji wako wa kilevi, kama unakunywa pombe kali,kunywa kinywaji kisichokuwa na mchanganyo kama Vodka , Konyagi na vinywaji vingine vikali.
Imeandikwa na @rabiadamary.
ConversionConversion EmoticonEmoticon