Kabla ya kukuelezea jinsi Wizkid alivyo rafiki na mastaa wawili ambao ni maadui wakubwa, turudi nyuma kwanza tuangalie jinsi ilivyoanza. Mlaumu Rihanna kwa kusababisha yote! Drake, Chris Brown na Rihanna waliwahi kujikuta kwenye kile wanachookiita ‘love triangle’ na hadi sasa mafahari hawa watatu hawakai tena zizi moja.
Uhusiano wa Chris na Rihanna ulianza mwaka 2008 licha ya kuwa marafiki tangia mwaka 2005. Hawakudumu sana, wakiwa kwenye kilele cha uhusiano wao mwaka 2009 waliachana baada ya Chris kumpiga Riri na kumpa kesi iliyomsumbua kwa takriban miaka sita. Lakini mwaka huo 2009 ndipo urafiki wa Rihanna na Drake ulianza na kuanza kuwepo kwa tetesi kuwa wana uhusiano.
May 2012 Drake alidaiwa kumdiss Riri kwenye wimbo No Lie kwa kurap: “Chances are if she was acting up then I f***ed her once and never f***ed again/ She could have a Grammy, I still treat her ass like a nominee/ Just need to know what that pussy like so one time is fine with me.”
Uhusiano wa Drake na Rihanna ulikuwa mkuki moyoni kwa Chris na hadi kufikia mwaka 2012 mastaa hao wawili walikuwa kwenye bifu kali. June 2012, Drake na Chris Brown walipigana kwenye klabu moja ya usiku huko New York na Breezy kupata mchubuko kwenye kidevu.
January 2013, Rihanna alithibitisha kuwa amerudiana na Brown kwa kusema: “When you add up the pieces from the outside, it’s not the cutest puzzle in the world. You see us walking somewhere, driving somewhere, in the studio, in the club, and you think you know. But it’s different now. We don’t have those types of arguments anymore. We talk about shit. We value each other. We know exactly what we have now, and we don’t want to lose that.”
April 2013, Drake alithibitisha kuwa Rihanna alikuwa chanzo cha bifu yao kwa kusema kwenye interview moja: At one point in life, the woman he [Chris Brown] loves fell into my lap.”
Hata hivyo, May 2013 Brown alithibitisha kuwa yeye na Rihanna wameachana tena.
Mwaka mmoja ulipita, hadi March 2014, ambapo Drake na Rihanna wakaanza kuwa karibu tena. Waliendelea kuwa karibu hadi January 27 ambapo Rihanna aliachia wimbo wake ‘Work’ aliomshirikisha Drake huku video yake ikionesha ukaribu wao tena. Drake pia amemshirikisha Riri kwenye wimbo wake ‘Too Good’ uliopo kwenye album yake mpya, Views. Bado wawili hao wameendelea kudaiwa kuurejesha uhusiano wao.
Wizkid ana bahati kubwa ya kuwa rafiki wa mastaa hawa wa Marekani wenye mashabiki wengi duniani. Alianza kuwa karibu na Chris Brown na hii ilikuwa ni baada ya Chris kwenda Nigeria December 2012. Huko Wizkid alikuwa miongoni mwa wasanii waliomsidindikiza kwenye show yake. Baada ya Breezy kurejea Marekani, alihojiwa kwenye kipindi cha 106 and Park cha BET na kuwaeleza jinsi ambavyo Wizkid alimfundisha kucheza style ya Azonto. Baada ya muda mfupi wawili hao walirekodi wimbo wa pamoja uitwao African Bad Gal ambao hadi leo haujawahi kutoka.
Baadaye kidogo, ukaribu wa Drake na Wizkid ukaanza. Wizkid alimshirikisha Drake kwenye remix ya wimbo wake Ojuelegba. Aliyewakutanisha wawili hao ni rapper wa Uingereza, Skepta ambaye yumo pia kwenye remix hiyo. Mwaka huu, Wizkid alishirikishwa na Drake kwenye wimbo One Dance ambao umeshika nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard 100 kwa wiki kibao.
Kwa kawaida, kama Chris Brown angekuwa na tabia za Kiswahili, angemuona Wizkid snitch kwa kuwa karibu na Drake hadi kushirikishwa kwenye album yake. Kuthibitisha hilo, Chris Brown alimuongeza Wizkid kwenye show zote za Ulaya za ziara yake ya ‘One Hell Hell of A Nite’ inayoendelea hadi sasa.
WIZKID AMEWEZAJE KUWA RAFIKI WA MASTAA HAO MAADUI?
Ni kwasababu kwa mtu mwingine lazima angejikuta anahamisha maneno huku na kule. Anapokuwa na Drake haleti story za Chris na anapokuwa na Chris haleti story za Drake. Hiyo ni sababu kubwa kwanini Mnaijeria huyo amekuwa kipenzi cha mastaa hawa wawili.
ConversionConversion EmoticonEmoticon