Timu ya taifa ya Brazil imekumbana na wakati mgumu katika mchezo wa Copa America 2016 dhidi ya Peru uliochezwa alfajiri ya June 13 2016, mchezo huo wa Kundi B ulikuwa unawapa nafasi kubwa Brazil kuibuka na ushindi, hususani takwimu ya kumiliki mpira kwa asilimia 66 ili wafanya Peru wacheze kwa kulinda goli zaidi.
Licha ya kuwa Brazil kuwa nafasi ya 7 katika viwango vya FIFA na Peru nafasi ya 48, walikubali kuruhusu goli dakika ya 75 baada ya Raul Ruidiaz kufanikiwa kufunga goli linaloaminika kuwa la mkono kwa wachezaji wa Brazil, goli hilo lilifanya mchezo kusimama na muamuzi kuvuta muda wa kufanya maamuzi.
Msimamo wa Kundi B
ConversionConversion EmoticonEmoticon