Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St Joseph waliokuwa wakisoma Kozi Maalumu ya Shahada ya Sayansi ya Elimu, wameruhusiwa kufungua kesi dhidi ya chuo hicho na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Ruhusa hiyo ilitolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, baada ya kuridhia maombi ya wanafunzi 316 yaliyowakilishwa na wenzao wanne; Ramadhani Kimenya, Faith Kyando, Oswald Mwinuka na Innocent Peter.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Elieza Feleshi baada ya mawakili wa Chuo cha St Joseph, Jerome Msemwa na wale wa TCU, Rose Rutta na Judith Misokia, kuridhia maombi hayo.
Source: Mwananchi
ConversionConversion EmoticonEmoticon