Akizungumza na Bongo5 wiki hii, Ben Pol amesema wimbo ‘Moyo Mashine’ ni wimbo ambao umefanya vizuri mapema zaidi kuliko nyimbo zake zote.
“Haijawahi kutokea nyimbo yangu ikafanya vizuri hivi kwa muda mfupi,” alisema Ben Pol “Moyo Mashine sasa hivi inakaribia view laki tano YouTube ndani ya wiki mbili na nusu sawa sawa na ‘Sophia’ ambayo ina mwaka na zaidi. Kwa hiyo hii ni historia kwa sababu haikuwahi kutokea katika maisha yangu ya muziki, kwa hiyo mimi nasema asante sana mashabiki wangu, media pamoja na watu wangu ambao nimefanya nao kazi au wameshiriki kwa namna moja kwenye project hii,”
- bongo5
ConversionConversion EmoticonEmoticon