Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amezidi kuingia kwenye headline ambapo asubuhi ya June 13 2016 alikutana na wanahabari na kuzungumzia kuhusu polisi kuzuia kongamano ambalo liliandaliwa na chama hicho ili kujadili bajeti pia alizungumzia kuhusu yeye kusakwa na polisi kwa kuviziwa na sio kwa utaratibu wa wito.
Jioni ya June 13 2016 Zitto Kabwe alipokea wito wa kuhitajika Central polisi kwa mahojiano ambayo yalichukua zaidi ya saa moja ambapo baada kutoka kwenye mahojiano aliyepata nafasi ya kuzungumza ni wakili wa chama hicho Steven Mwakibolwa ambaye ameeleza sababu za wito huo kituoni hapo……..
>>> wamechukua statement ya Zitto kufuatana na kongamano la chama lililokuwa limezuiliwa jana kwa sasa baada ya mahojiano na mazungumzo na polisi, chama kitatoa taarifa rasmi kufuatana na nini kitafuta baada ya hapa’
>>> kama alivyoeleza mwanasheria tumemaliza mahojiano na polisi kwa hiyo kesho tutatoa kauli yetu ya hatua inayofuata, nimeitwa polisi nimekuja, wanachama watulie tunaendeleamajadiliano na polisi ili tuendelee na kazi zetu za kisiasa kama kawaida’-Zitto Kabwe
ConversionConversion EmoticonEmoticon