Klabu ya Azam FC jana imezindua duka lake jipya lililopo ndani ya boti za Azam Marine litakalokuwa linauza vifaa vya michezo vya timu hiyo.
May 24 timu hiyo ilifanikiwa kuzindua duka lake la kuuza vifaa vya michezo maeneo ya Kariakoo na sasa imekuwa timu ya kwanza Tanzania kuzindua duka lake ndani ya boti.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuzindua duka hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa timu hiyo, Saad Kawemba amesema wameamua kufungua duka kutokana na kuwarahisishia mashabiki wao wanaosafiri kuelekea Unguja na Pemba kuvipata vifaa hivyo vya michezo na wale wasiopafahamu Kariakoo eneo lililopo duka lao kuu.
“Tumeamua kufungua duka letu jingine la vifaa vya michezo lililopo ndani ya boti zetu na kuuza jezi zetu pia ili kurahisisha upatikanaji wa jezi hizo ambapo tunataka msimu mpya utakapoanza mashabiki wetu wataqkapo kuja uwanjani kutushangilia waje wakiwa wamevaa jezi ya timu yetu,” alisema Saad.
“Kwa sasa hatuongei chochote kuhusu Azam FC tumemsajili nani wala tunafanya nini ila mambo yatakapo kamilika tutawafahamisha nini kilikuwa kinaendelea,” aliongeza.
Aidha Kawemba aliongeza jezi zao ni original kabisa ni sawa sawa ile anayoivaa Pascal Wawa anapokuwa uwanjani tofauti na timu nyingine duniani zinavyofanya.
- bongo5
ConversionConversion EmoticonEmoticon