Wenger: Kante ni mchezaji adimu

Arsene Wenger amemwagia misifa tele N'Golo Kante kama mchezaji shupavu, mahiri na wakipekee amabaye anamkubali sana
Kiungo huyo wa Leicester City alifanya maajabu katika msimu wake wa kwanza Ligi Kuu Uingereza, akiisaidia timu yake ambayo ilikuwa haipewi nafasi kubwa kutwaa ubingwa, klabu nyingi zimeonesha nia ya kutaka kumsajili.

Goal inafahamu kuwa Arsenal wamefanya mazungumzo na nyota mwingine wa Leicester, Jamie Vardy baada ya kuwa tayari kutoa paundi milioni 20 kununua mkataba wake na Wenger amebainisha sasa kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa Kante.

"Namkubali sana na ninampenda N'Golo Kante. Ana mbinu tele," Wenger alikiambia beIN Sports.

"Ni mchezaji wa kipekee sana kwa soka la Ulaya. Ana ubora wa aina yake. Ana hisia za soka, ni watu wachache sana wanaweza kuwa kama yeye. Daima yupo anapotakiwa kuwa na anafanya anachopaswa kufanya."

"Ni adimu sana kuwa na kiungo wa kati kama yeye. Si kwa upande wa kushoto tu lakini kulia pia."

Kante ametajwa kwenye tetesi za kuwa kwenye rada za Paris Saint-Germain na kwa sasa yupo kwenye kikosi cha Ufaransa kinachoshiriki Euro.

By Meshack Brighton
Previous
Next Post »