Kazimoto alikutwa na kesi hiyo ya kumpiga vibao Mwanahiba wakti Simba ilipokuwa kwenye mazoezi uwanja wa CCM Kambarage mkoano Shinyanga
Kiungo wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania Mwinyi Kazimoto ameachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga baada ya kukutwa hana hatia kufuatia shitaka la kumpiga Mwandishi wa Kampuni ya Mwanachi Communications Limited Mwanahiba Richard.Kazimoto ameiambia Goal, Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo iliyotokea Febuari 10, 2016, mkoani Shinyanga Rahim Mushi, kumpa ushindi Kazimoto kwa madai hakuwa na kosa na kulimaliza swala hilo lililokuwa likimsumbua kiungo huyo.
“Nashukuru Mahakama imenikuta sina hatia na kesi imemalizika ni jambo ambalo lilikuwa wazi lakini kwasababu lilishafika kwenye vyombo vya sheria lakini nafurahi kuona yamekwisha na mimi nimeshinda ingawa mwenzangu ametakiwa kukata rufaa kama hajaridhika,”amesema Kazimoto.
Kazimoto alikutwa na kesi hiyo ya kumpiga vibao Mwanahiba wakti Simba ilipokuwa kwenye mazoezi uwanja wa CCM Kambarage mkoano Shinyanga ilipokwenda kucheza mechi mbili dhidi ya Kagera Sugar na wenyeji Stend United ambapo ilishinda mechi zote mbili.
- By zuberi Karim Jumaa
ConversionConversion EmoticonEmoticon