Waandaaji wa tuzo za BET wametangaza kumpatia Akon tuzo ya heshima ya Global Good kwenye tuzo zitakazofanyika Los Angeles, Juni 26 mwaka huu.
Waandaaji wa tuzo hizo za BET wameamua kumpatia tuzo hiyo ya heshima Akon kutokana na mchango wake anaoutoa wa kuleta maendeleo kwenye bara la Afrika kutokana na mradi wake wa umeme wa jua ‘Akon Lighting Africa’ ulioanza kazi mwaka jana huku akipanga kusaidia zaidi ya watu milioni 600.
Tuzo hiyo ilianza kutolewa mwaka jana kwa watu wanaotoa mchango mkubwa wa kuleta maendeleo kwenye bara la Afrika na mtu wa kwanza kupatiwa tuzo hiyo alikuwa ni Miss Tanzania 2001, Millen Magesse.
ConversionConversion EmoticonEmoticon