Watoto wawaunganisha tena Nick Cannon na Mariah Carey


Rapper wa Marekani, Nick Cannon na Mariah Carey waliweka tofauti zao pembeni na kuonyesha upendo kwa watoto wao kwa kusherehekea kwa pamoja siku ya Baba Duniani japo wametengana.
Nick Cannon alisherehekea siku ya Baba Duniani akiwa na mzazi mwenzake, Mariah Carey watoto wao, Monroe na Moroccan.
Kupitia akaunti ya instagram, Nick Cannoa aliandika: “Leaving the Haters in the Wind! LOL They want us to be mad so bad! @MariahCarey but we happier than happy! #HappyFathersDay.”
Nick Cannon na Mariah Carey walifanikiwa kufunga ndoa mwaka 2008 lakini waliachana mwezi Agosti, 2014. Hivi karibuni Nick Cannon ameachia wimbo wake mpya ‘Divorce Paper’ ambao unalinganishwa na tetesi za kukataa kusaini makaratasi ya talaka.

Kwa sasa Mariah Carey ndiye anakaa na watoto hao kutokana na amri ya mahakama na tayari yupo kwenye mipang ya kufunga ndoa na James Packer.
Previous
Next Post »