Donald Trump ameshatumia $55m kutoka mfukoni mwake kwenye kampeni za Urais Marekani


Kama akishindwa uchaguzi wa Marekani, Donald Trump atakuwa mgombea aliyepoteza zaidi.
Ni kwasababu hadi kutajwa kuwania urais wa mwaka huu kupitia chama chake cha Republican, bilionea huyo ametumia dola milioni 55 zake mwenyewe kugharamikia kampeni zake.
Akiongea wiki hii, Trump amesema haoni tatizo iwapo atatumia tena fedha zake mwenyewe kugharamikia kampeni za uchaguzi huo mkuu ambapo anachuana na Bi. Hillary Clinton.
“I spent $55 million of my own money to win the primaries. 55, that’s a lot of money by even any standard,” alisema Trump said. “I may do that again in the general election.”
Aliongeza kuwa pamoja na kwamba fedha aliyonayo ni nyingi kutosha kufanya mwenyewe, ni vyema akapewa msaada na chama pia.
Hadi sasa Trump amekusanya dola milioni 1.3.
Mpinzani wake, Clinton wa chama cha Democratic yuko vyema. Hadi sasa amekusanya zaidi ya dola milioni 42. Clinton na wadhamini wake wanatarajia kutumia dola milioni 117 kwaajili ya matangazo ya TV tu.
Previous
Next Post »