Danny Msimamo: Vinega na Anti Virus Imebadili Game



Msanii wa Hip Hop wa hapa bongo Danny Msimamo, amesema game la muziki sasa hivi limebadilika tofauti na zamani, ambapo sasa muziki unaingiza pesa nyingi kwa wasanii.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Danny Msimamo amesema hatua hiyo imesababishwa na harakati za kutetea haki zao na kuendeshwa kwa kampeni mbali mbali kama Vinega na Anti Virus.

“Sasa hivi iko poa watu wamekuwa wakifunguka tofauti na mwanzo, watu wanapata hela nyingi kidogo, mwanzo ilikuwa ni ngumu, lakini baada ya kupiga kampeni mbili mbili tatu, anti virus, kufungua fungua mambo atleast sasa hivi wanapata hela, mwanzo ilikuwa ni ngumu msanii kulipwa hata milioni, sasa hivi watu wanapata milioni tano, kumi, muziki unalipa siku nyingi sema watu walikuwa hawajafunguka”, alisema dany msimamo.

Danny Msimamo aliendelea kusema kuwa hapo mwanzo watu walipo kwenye tasnia ya muziki walikuwa wanawabania wasanii na kusababisha kipato hafifu, huku wakilazimika kutumia pesa zaidi ili waweze kufanikiwa.

“Wadau walikuwa wanabana, kuna hawafanyishughuli yoyote, haimbi hafanyi nini lakini yupo kwenye muziki na anapata hela, sasa inabidi ufanye kazi, toa hela na wewe upate hela.

- source eatv.tv
Previous
Next Post »