Wakati Ufaransa wanapojiandaa kuikabili Romania katika mechi ya kwanza Euro 2016, ni vigezo vipi vinaweza kuwapa ushindi au kushindwa?
PREVIEW
Ufaransa na Romania zitaanza kukipiga Euro 2016 mjini Paris Ijumaa usiku wenyeji wakipewa nafasi kubwa kuanza kampeni hizo kwa ushindi.
Michuano mikubwa hata hivyo si rahisi, na Les Bleus watakuwa wanajua ubora wa Romania katika kumiliki mpira dimbani, wachezaji kadhaa wakiwa wanacheza katika klabu bora za Ulaya.

Vita zipi basi zitanoga katika mechi hiyo itakayopigwa Stade de France?
Olivier Giroud vs. Vlad Chiriches
Giroud ataiongoza safu ya mashambulizi ya Les Bleus na atakabiliana na beki wa zamani wa Tottenham Chiriches.
Uchezaji wa asili wa Giroud utakifaa sana kikosi cha Ufaransa kwani Deschamps anapenda mashambulizi ya nguvu, mbinu ambayo wakati mwingine inatumiwa na Arsenal.
Chiriches atahitaji kutumia nguvu zake na uwezo wake wote kuusoma mchezo na kumnyamazisha mshambuliaji huyo hatari wa Ufaransa.

Bacary Sagna vs. Bogdan Stancu
Kwa timu hiyo mpya na mahiri, si jambo jema sana kuwategemea mabeki Patrice Evra mwenye umri wa miaka 35 na Sagna mwenye umri wa miaka 33. Kuruhusu mashambulizi kutaleta madhara.
Beki wa Manchester City, Sagna atakuwa kichochoro iwapo atashambuliwa kwa malengo, kumzuia kupanda kwani ni mdhaifu katika swala la kasi.
Stancu ni mchezaji mahiri, mshambuliaji mwerevu anayeweza kuwaletea Ufaransa madhara.Adil

Rami vs. Florin Andone
Ni dhahiri kwamba Romania watatumia muda mwingi wa mechi yao kukaba, kwani watahitaji kukabiliana vikali dhidi ya mashambulizi ya jeshi la Ufaransa. Lakini wanaweza kupata fursa chache ambazo ni lazima Andone atahitaji kuzitumia vizuri na kwa usahihi zaidi.
Mshambuliaji huyo wa Cordoba atakabiliana na Rami ambaye nafasi yake kwenye timu ina walakini kwani ni mchezaji anayeweza kufanya makosa mengi zaidi katika kikosi cha Ufaransa.
VIKOSI
Ufaransa: Lloris, Sagna, Rami, Koscielny, Evra, Pogba, Kante, Matuidi, Coman, Payet, Giroud
Romania: Tatarusanu, Sapunaru, Chiriches, Grigore, Rat, Pintilii, Hoban, Torje, Stanciu, Stancu, Andone

- by Meshack Brighton
ConversionConversion EmoticonEmoticon