Rapper kutoka Marekani, Desiigner amewashangaza mashabiki baada ya kutangaza kuachia mixtape yake mpya ‘New English’ kwa ajili ya mashabiki wake huku akiwa tayari alitangaza ujio wa albamu yake mpya mwaka huu.
Desiigner ni mmoja kati ya wasanii kutoka lebo ya G.O.O.D Music inayomilikiwa na rapper, Kanye West wimbo wake wa ‘Panda’ umezidi kufanya vizuri mpaka kufikia namba moja kwenye chati za Hot 100 nchini Marekani.
Albamu mpya ya Desiigner aliyotangaza mwezi uliopita ataiachia mwaka huu ni ‘The Life Of Desiigner’ ikiwa inafanana na jina la albamu ya mwisho ya bosi wake, Kanye West ‘The Life Of Pablo’.
ConversionConversion EmoticonEmoticon