Katika ulimwengu wa mitandao ya kijamii moshi wa uhusiano wa mastaa huanza kufuka kwa posts kwenye mitandao ya kijamii.
Zuu aka Jipe Shupa akiwa na mpenzi wake Max Spesho
Vivyo hivyo staa wa tamthilia ya Kelele ya Clouds TV, Max Spesho na video vixen aliyetumika kwenye video ya wimbo wa Nuh Mziwanda, Jike Shupa wameonesha kuwa na kitu. “Wengi wananijua ila huyu ananijua zaidi.@jike_shupa my special,” aliandika Max kwenye Instagram.
Nimemuuliza Max kama kuna lolote na hakuwa mchoyo wa kuweka mambo hadharani. “Ni kweli ni mpenzi wangu na tunapendana kweli kama mke wangu,” Max ameiambia Bongo5.
Futari na bae
“Zuu namchukulia kama mwanamke ambaye anatazama mbele zaidi kimaisha hasa kimawazo sababu toka nimekuwa naye kila siku ananipa mbinu mpya za maisha hasa katika sanaa ninayoifanya hata yeye mwenyewe amekuwa akijipanga kila siku kupanda katika maisha yake sio kwangu,” ameongeza.
“Namchukulia Zuu kama mwanamke anayeniletea ubunifu n akukaza kataka maisha yang nampenda sana kiukweli.”
Zuu ametokewa kuwa maarufu tangu aonekana kwenye video ya Nuh Mziwanda hasa kwasababu anafanana mno na Shilole.
“Of course anafanana na Shishi lakini kwa upande wetu mimi na yeye tunasema Shishi ndio kafanana na Zuu, sio Zuu kafanana na Shishi,” anasema.
“Of course anafanana na Shishi lakini kwa upande wetu mimi na yeye tunasema Shishi ndio kafanana na Zuu, sio Zuu kafanana na Shishi,” anasema.
Like Shilole like Zuu
“Kila sehemu nikitoka naye watu wanajua Shishi mpaka kuna siku msanii mmoja alikuja akamuona sehemu akidhani kuwa ni Shilole tukabakia tu kucheka naye kujishtukia.”
ConversionConversion EmoticonEmoticon