Miaka kama miwili iliyopita, AY kupitia kampuni yake ya Unity Entertainment alikuwa akisimamia wasanii
Miongoni mwa wasanii waliofanya kazi na kampuni hiyo ni pamoja na Ommy Dimpoz, Feza Kessy na Stereo. “Sasa hivi nimeamua kuangalia kwenye kona nyingine zaidi kuliko ku-manage artists,” AY ameiambia Bongo5.
Anasema mikataba ya Ommy na Stereo iliyokuwa ya mwaka mmoja iliisha na amedai kuwa hawakuwahi kuwa na tatizo. Hata hivyo mkataba wa Feza Kessy ulivunjika kutokana na kushindwa kuzingatiwa kwa baadhi ya vipengele vya mkataba.
“Kuna vitu vilinikatisha tamaa nikaamua kuachana na hiyo kitu ya kusimamia wasanii. Ndio maani nilimrecruit Sallam, ndio maana anaendelea kufanya hizo kazi mimi nimerudi nyuma kidogo,” ameongeza.
Sababu kubwa ambayo AY anadai kumkatisha na tamaa ni kile alichosema ‘wasanii hawaheshimu signature zao.’
Ushauri wa AY kwa wasanii wengine wenye nia ya kusimamia wasanii wenzao ni kuhakikisha wanamchukua msanii smart. Amesema tatizo kubwa ni pale ambapo unaweza kumjenga msanii akawa mkubwa lakini akaja kudanganywa na watu wengine akaamua kuondoka kinyemela.
Amesema kwa sasa hana mpango tena wa kurejea kwenye kazi hiyo na kwamba kwa sasa atakuwa akitoa tu ushauri na kuwapa njia za kupitia wasanii wengine.
- source bongo5
ConversionConversion EmoticonEmoticon