Video ya wimbo ‘Jike Shuka’ ya Nuh Mziwanda yamtoa povu Ex wake, Shilole

Video queen wa video ya wimbo ‘Jike Shupa’ anayedaiwa kufanana na Shilole akiwa na Nuh
Ikiwa ni siku chache toka Ex wa Shilole, Nuh Mziwanda aachie video ya wimbo ‘Jike Shupa’ ambayo inaelezea jinsi alivyoishi na mpenzi wake huyo, Shilole ameonyesha kukasirishwa na kazi hiyo.

Nuh amethibitisha kwamba Shilole ndiye aliyemuimbia kwenye wimbo huo, kwa kumtumia video queen anayefanana na Shilole kama pacha katika video ya wimbo huo.

Sholole baada ya kuona video hiyo, aliandika ujumbe instagram ambao baadae aliutoa:

Wale unaongozana nao wanaweza kuwa mizigo au Baraka. Shukrani za dhati kwani kwenye mashabiki zangu ambao ni baraka na pole sana wasanii wote mnaodhani bado tupo dhama za kutumia mgongo wa mtu mwingine kuweza kutoboa. Kipaji siyo maneno ila ni vitengo. Umemiss mkong’oto?. Sipendagi mwanaume mjinga ndiyo maana umekula mkong’oto wa kutosha… Mshamba usiyejua hata kubadilisha boxer, niweke mbali na maisha yako. Nikifungua mdomo wangu utadhalilik

Shilole na Nuh Mziwanda waliachana miezi kadhaa iliyopita ambapo Nuh amekuwa alizungumzia mengi yaliyomkuta wakati akiwa kwenye mahusiano na mwanadada huyo, huku Shilole akitaa kuzungumzia kilichotokea.



Previous
Next Post »