Belle 9 anatarajia kuachia remix ya hit single yale ‘Burger Movie Selfie’ siku chache zijazo
Nimepiga naye story na amenieleza mambo haya manne makubwa kuhusiana na remix hiyo.
1.NI REMIX YAKE YA KWANZA
Belle 9 ni miongoni mwa wasanii wa R&B Bongo waliowahi kuachia single kali zilizosumbua redioni na kwenye TV. Nyimbo kama Sumu ya Penzi, Masogange, We ni Wangu aliomshirikisha Mr Blue na zingine nyingi zilikuwa anthem kwa muda mrefu. Hits hizo zimempa nafasi ya pekee muimbaji huyo wa Morogoro kwenye muziki wa Bongo Flava. Pamoja na kuwa na hits zote hizo, hajawahi kufanya remix ya wimbo wake wowote. Remix ya Burger Movie Selfie inakuwa ya kwanza kwenye career yake. Kwa BMS umekuwa wimbo special unaohitaji special treatment. Anadai maombi ya remix ya wimbo yalikuwa makubwa si tu kwa mashabiki wake, bali pia wasanii wenzake waliotamani kuweka vionjo vyao humo.
2. AMESHIRIKISHA WASANII WATANO
Remix ya BMS inakuja kuingia kwenye historia ya kuwa remix ya R&B iliyoshirikisha wasanii wengi kwa pamoja. Ukimtoa yeye, kuna wasanii watano wengine amewashirikisha akiwemo muimbaji mmoja wa kike.
3.AUDIO IMETAYARISHWA NA WATARISHAJI WANNE TOFAUTI
Belle amenieleza kuwa remix ya wimbo wake imeguswa na mikono ya watayarishaji mahiri wanne. Wa kwanza ni Tiddy Hotter aliyetengeneza origina version. Wengine ni Ema The Boy, Tudd Thomas na Chizan Brain. “Ilitoka One Love Records kwa Tiddy ikaenda Epic Records kwa Ema The Boy na Tudd Thomas, ikaenda kumaliziwa B Records kwa Chizan Brain. But executive producer ni Tiddy Hotter,” anasema Belle. You can imagine kwa ujuzi wa watayarishaji wote hao remix ya BMS itakuaje!
4. VIDEO IMEONGOZWA NA WAONGOZAJI WATATU
Video ya wimbo huu pia imepitia mikono ya waongozaji watatu mahiri. Alimsafirisha Mkenya, Enos Olik kuja Bongo kushoot kichupa hicho huku akipata usaidizi wa hapa na pale kutoka kwa Hanscana na Khalfan.
-source bongo5
ConversionConversion EmoticonEmoticon