Seyi Shay almanusra akiwekee mchanga kitumbua cha Wizkid. Muimbaji huyo wa Nigeria alikuwa nchini Jamaica alikoenda kwa ziara ya kikazi na katika moja ya interview alizofanya alijikuta akiongea kitu ambacho baadaye kimekuja kumtokea puani.
Kwenye interview hiyo na kipindi cha On Stage, mtangazaji alimuambia Seyi kuwa kuna mjadala unaendelea Jamaica kuhusu Drake kuchukua vionjo vya dancehall kwenye nyimbo zake.
Pasipokujua ukali wa kauli yake, Seyi alifunguka: Mjadala huo huo unaendelea Afrika kwa sasa kwamba [Drake] anasample afrobeat. Kwasababu [One Dance] kiukweli ni wimbo wa Wizkid kwahiyo sio wimbo wa Drake. Wizkid aliuandika na watayarishaji wengine wa Nigeria waliutayarisha kama wimbo wa Afrobeat na wakatoa vitu vingi na kuacha rhythm na rhythm ndiyo inayoifanya reggae na afro beat na ragga na muziki wa Afrika ufanane.”
Wizkid aliyeshirikishwa na Drake kwenye wimbo huo uliopo kwenye album yake Views, alichukizwa vikali na kauli ya Seyi Shay na kuamua kujibu kwenye Twitter.
“She lied,” alianza kwa kumjibu shabiki mmoja. “Don’t say what you know nothing about! Shut up,” alitweet.
“I don’t need to explain my business to no one. Listen to my music and enjoy. Just know we getting cheques though.”
“I don’t need to explain my business to no one. Listen to my music and enjoy. Just know we getting cheques though.”
Pamoja na yote yaliyotokea, Wizkid alisema hana tatizo na Seyi Shay.
Seyi Shay alikubali kuteleza ulimi na kuomba radhi huku akidai kuwa alitoa kauli hiyo kwa kusikia maneno ya mtaani.
Hata hivyo mambo yanazidi tu kumnyookea Wizkid ambaye ametweet kueleza kuwa kuna collabo na Swizz Beatz inakuja:
ConversionConversion EmoticonEmoticon