Mkongwe wa bongo flava Mwanadada Mwasiti amefunguka na kusema kwamba wimbo wake mpya wa Utabaki unaniangalia hauhusiani kabisa na maisha yake ya kimahusano na amesema huo ni wimbo kama nyimbo nyingine na kwamba yeye haimbi kwa kumlenga mtu.
Hata hivyo Mwasiti ameiambia Enews kwamba hana mahusiano ya kimapenzi na mtangazaji maarufu hapa nchini Sam Misago wa EATV ambapo amesema kuwa yeye na Sam ni washkaji wa muda mrefu takribani miaka saba iliyopita na kuomba mashabiki zake wajue kuwa yeye ni mchumba wa mtu ambaye sio maarufu.
Mwasiti aliendelea kusema kwamba anaomba mashabiki zake wasimuelewe vibaya kwani hapo awali aliahidi kutoa wimbo wake wa HIP HOP lakini imekuwa tofauti kutokana na Fid Q kushindwa kumuandikia mistari kwa wakati kama alivyokuwa ametarajia.
eatv.tv
ConversionConversion EmoticonEmoticon