Kuna wizi mpya mjini.. si wa magari au fedha ni wa akaunti za Instagram!
Wizi huo umepamba moto na wahanga wakubwa ni wasanii. Baada ya Linah ambaye hadi leo akaunti yake ya Instagram imeenda na maji, Joh amekuwa mhanga wa mpya lakini yeye amebahatika kuikomboa.
“Watu wa Mungu nimefanikiwa kuirudisha ofisi yetu hii lakini sasa sio tena kwa jina la zamani wajanja washaliwahi. Kwa sasa ni follow humu @johmakinitz.”
Hata hivyo followers wake wamebaki kuwa wale wale. Hadi sasa anao zaidi ya 880k. Akaunti yake ya mwanzo ilikuwa na jina la @joh_makini.
Hata hivyo kuna tetesi pia kuwa baadhi ya watu wakimewemo mastaa, wamekuwa na mtindo wa kuuza akaunti zao kwa watu wanaozinunua kufanyia biashara ya matangazo na wao kuanzisha zingine.
ConversionConversion EmoticonEmoticon