Kiungo mkongwe wa Manchester United, Michael Carrick ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuichezea Manchester United chini ya kocha mpya, Mreno Jose Mourinho.
Huku wengi walikuwa wakiamini itakuwa vigumu kupewa nafasi chini ya kocha Jose Mourinho.
Kiungo huyo mwenye miaka 34, amekuwa uti wa mgongo wa kiungo cha timu hiyo ambayo ni mabingwa wa Kombe la FA.
Carrick alijiunga na Man United kwa mara ya kwanza mwaka 2006 akitokea Tottenham mwaka 2006, amekubali kuongeza Mkataba utakaomuweka Old Trafford hadi Juni 2017 kukamilisha miaka 11 ya kuwatumikia Mashetani Wekundu.
Katika kipindin chake cha miaka 10 Man United hadi sasa, mchezaji huyo ameshinda mataji matano ya Ligi Kuu, Kombe la FA, Kombe la Ligi moja, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA.
ConversionConversion EmoticonEmoticon