Nani anamzomea Gerard Pique sasa?

Pique na Iniesta walifanya ushirikiano mzuri kuipatia ushindi Hispania japo kwa taabu dhidi ya Jamhuri ya Czech katika mchezo uliopigwa Toulouse Jumatatu.


Nani anayemzomea Gerard Pique sasa? Amekuwa mtu wa kudhihakiwa na kupigiwa miluzi na mashabiki wengi wa Hispania kwa sababu ya kuiponda Real Madrid pia na asili yake ya Catalan, lakini alikuwa shujaa wa La Roja Jumatatu, akiunganisha pasi safi kutoka kwa Andres Iniesta dakika za majeruhi.

Hispania imeanza vizuri kampeni za kutetea taji lake katika michuano ya Euro 2016 kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuichapa Jamhuri ya Czech.

Bao la kichwa la dakika za lala salama lilofungwa na mlinzi Gerard Pique akiunganisha krosi ya Andres Iniesta hatimaye lilipeleka faraja kwa wahispania kufuatia upinzani mkali walioupata kutoka kwa wapinzani wao.

Alvaro Morata, Jordi Alba na David Silva juhudi zao ziligonga mwamba huku mabingwa hao watetezi wa taji la Ulaya wakishindwa kufunga katika dakika za mapema na kusubiri hadi dakika za jioni.

Safu ya mashambulizi, MSN ya Hispania ilihangaika kuivunja ngome ya Jamhuri ya Czech. Silva alimtengea mpira safi Morata kipindi cha kwanza, lakini mshambuliaji huyo wa Juventus alimpigia moja kwa moja Petr Cech, Na mlinda mlango huyo wa Arsenal hakuchelewa kumzuia Silva kufunga na aliokoa hatari kutoka kwa Morata na Iniesta.

Iniesta alikuwa injini ya mchezo. Kiungo huyo wa Barcelona alikuwa kila mahali: akijitahidi kupenya safu ya kiungo na ulinzi ya wapinzani, akipiga pasi nzuri za kiufundi ndani ya eneo lao. Lakini pamoja na yote hakuweza kufanya lolote, washambulizi wa Hispania walicheza chini ya kiwango. Mwendo wa Morata ulikuwa mzuri, lakini hakuonesha umahiri wake. Baadaye alipotolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Aritz Aduriz, Kikosi cha Del Bosque kilionekana kufaidika na mabadiliko.

Hispania pia ilinurusika kuchapwa bao pale Cesc Fabregas alipookoa mpira kwenye mstari wa goli uliopigwa na Theodor Gebre Selassie

Vladimir Darida alipata nafasi ya kuisawazishia Jamhuri ya Czech lakini mlinda mlango wa Hispania David de Gea alikuwa vizuri langoni licha ya tuhuma zinazomkabili.

-By Meshack Brighton

ConversionConversion EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng