PICHA:One Love Record ya Tiddy Hotter kumtambulisha msanii mpya weekend hii.





Record label mpya inayofahamika kama ‘One Love Record’ chini ya producer Tiddy Hotter inatarajiwa kumtambulisha msanii mpya wekeend hii ikiwa ni pamoja na ku-release kazi ya kwaza ya msanii huyo ambayo imeandaliwa kwenye studio za ‘One Love Record’ na producer Tiddy Hotter.

Akizungumza na Teamtz.com Tiddy Hotter ambae amefanya kazi na wasanii kama Ben Pol,Belle9,Godzila,G-Nako,Fid-Q na Stamina amedai kuwa awali alikua akifanya shughuli zake za kimuziki mkoani Mwanza ila ameamua kuhamishia makazi yake Dar es salaam na kufungua studio yake iliyopo maeneo ya Survey-Makongo juu na kuongeza kuwa mpaka sasa ameshafanya kazi na wanamuziki wakubwa nchini ila kwa mara ya kwanza amekusudia kumtambulisha msanii mpya ikiwa ni pamoja na nyimbo yake ambayo itakua kazi ya kwanza kutoka kwenye record label hiyo anayoimiliki.

TIDDY HOTTER NA SOUDY BROWN 001        Tiddy Hotter(r)akiwa na  Co-Host na Producer wa kipindi cha XXL cha Clouds Fm,Soudy Brown.
“nimefanya kazi na wanamuziki wakubwa wengi tu tangu nifungue studio yangu mpya ila siwezi kuwataja kwa sasa coz plan yangu kwanza ni kuleta vipaji vipya kwenye muziki wetu wa kitanzania ….as to prove that nimeamua kuanza na Mdadisi,watu wengi hawamfahamu ila trust me kuna kitu kwa huyu jamaa na naamini watu watafurahia kazi hii ambayo nimeianda kwa mikono yangu….nyimbo yake itatoka rasmi tarehe 11-06-2016,i mean jumamosi hii na itapatikana mtandaoni pia”.Alidai Tiddy Hotter.

TIDDYHOTTER NA BELLE 9

                                       Tiddy Hotter & Belle9 @One Love Record.
MDADISI                                                                 Mdadisi.

BEN PAUL ON MDADISI 02
BARAKA DA PRINCE ON MDADISI 001
Ikumbukwe kuwa Tiddy Hotter ndie alietengeneza hits kama “Burger,Movie & Selfie” ya Belle9,na “Nisome” ya Godzila na G-Nako.

Previous
Next Post »