Promota wa Nigeria aishitaki Roc Nation na Rihanna kwa kutotokea kwenye show iliyotakiwa kufanyika mwaka 2013



Roc Nation na Rihanna wamefikishwa kortini na muandaji wa matamasha wa Nigeria aliyewashitaki kwa kutotokea kwenye show iliyotakiwa ifanyike mwaka 2013 japo aliwalipa.

Promota huyo anayejulikana kwa jina la Chris Ubosi, amemumbuluza muimbaji huyo wa ‘Work’na label yake Kortin kwa madai ya kuwa alilipa Dola 425,000 kwa ajili ya show hiyo ambayo Rihanna alitakiwa atumbuize kwa dakika 65 tu lakini hakutokea.

maxresdefault (2)

Promota huyo amedai kuwa aliongea na wawakilishi wawili wa Rihanna,na lebel yake ya Roc Nation inayomilikiwa na Jay Z na kuwalipa kiasi icho cha pesa, amesema show hiyo iliyotakiwa ifanyike May ilisogezwa hadi Julai baada ya wawakilishi hao kuomba asogeze mbele lakini cha ajabu hakuna aliyetokea hadi leo.

Ubosi anataka kulipwa Dola laki 1.6, Hata hivyo Roc Nation imekanusha kufanya mzungumzo yoyote na Promota huyo.

-by 
Previous
Next Post »