Hans Poppe yupo Zimbabwe kwa ajili ya kufanikisha mipango ya kumsajili Kalisto Pasuwa lakini pia wanatafuta suluhisho la beki baada ya kuondoka kwa Juuko Murshid
Baada ya kukaribia kumnasa kocha wa timu ya taifa ya Zimbabwe Kalisto Pasuwa, uongozi wa Simba umeanza mazungumzo na beki wa kati wa Black Leopards ya Afrika Kusini raia wa Malawi Harry Nyirenda kwa lengo la kumsajili kuichezea timu hiyo msimu ujao.
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hans Poppe, ameiambia Goal, wana tatizo na beki wa kati baada ya kuondoka kwa Juuko Murshi na Nyirenda ndiyo wanaamini atakuwa mtu sahihi kwenye nafasi hiyo.
“Nimevutiwa na uwezo wake akiwa na timu ya taifa ya Malawi ilipocheza na Zimbabwe nadhani anaweza kuwa msaada kwetu kama tutafanikiwa kumpata ili kusaidiana na Novaty Lufungo,”amesema Hans Poppe.
Hans Poppe yupo Zimbabwe kwa ajili ya kufanikisha mpango wa kumsajili kocha Pasuwa kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo msimu ujao kuziba pengo la Mganda Jackson Mayanja.
By Zuber Karim Jumaa