Mzee Abdul amelazimika kwa miaka mingi kushuhudia tu mafanikio makubwa ya mwanae Nasib aka Diamond Platnumz akiwa mbali naye.
Pamoja na jitihada zake zote za kumshawishi mwanae awe muumini wa ile methali isemayo ‘yaliyopita si ndwele tugange yajayo’, bado ameendelea kukutana na ukuta! Inajulikana, Mzee Abdul aliwatelekeza Diamond na mama yake na kuwafanya waishi maisha ya tabu kwa miaka mingi.
Mungu hamtupi mja wake, Diamond akafunguliwa milango na leo hii si tu msanii mkubwa Afrika, bali pia ni tajiri mkubwa – Chibu katusua hasa!
Majuto ni mjukuu, leo hii Mzee Abdul ameendelea kuishi maisha ya kubangaiza, kuugua lakini yote hiyo haijamfanya mwanae alegeze uzi.
Lakini kwa ujumbe wa Father’s Day, huenda hitmaker huyo wa ‘Make Me Sing’ akawa ametafuta sehemu ndogo kwenye moyo wake na kuukumbuka uwepo wa mshua wake na kumshukuru kwa kumleta duniani, kwasababu mwisho wa siku bado ni baba yake.
Japo haikuwa rahisi kuweka picha ya baba yake, Diamond aliandika: To my Dad…My Self and my all fellow Fathers in the world.”
Unadhani kuna siku Diamond atakuja kuwa karibu tena na baba yake? comment hapa chini
ConversionConversion EmoticonEmoticon