Wazee wa zamani wana msemo unasema wivu kidonda , sio uongo kuwa na wivu si jambo baya sana ila wivu uliopitiliza ni ugonjwa, na wivu husababishwa na wasiwasi wa kumpoteza ulie nae kwa mtu mwingine, hii inafanya mtu kutokuwa na imani na mpenzi wake hata kama akitoka kwa dakika chache tu.
Nasema wivu ni ugonjwa kwa nini, wivu unaweza sababisha ugomvi, wivu unaweza leta maumivu kwako au hata kwa mpenzi wako, ndugu jamaa na marafiki wivu unaleta chuki na hata wengine kuchukia mapenzi nakuamua kuwa pekeyao, tayari inaleta matatizo ya kisaikolojia
Nini Ufanye kuzuia wivu uliopitiliza
- Mwamini mwenza wako
Inawezekana ikawa ni kazi ngumu kidogo lakini, hakuna dawa nzuri ya wivu kama kuamini mpenzi wako ni muaminifu na hawezi kukusaliti hata kama unajua ni ngumu kujipa moyo jua ya swala hilo.
- Acha kujifananisha na wengine
Usijaribu kujifananisha na wengine, wakati mwingine wivu pia unaanzia kwa mtu mwenyewe kutojiamini sababu anajiona havutii kama wanawake/wanaume wengine na pengine anashangaa kwanini mwanaume Yule au mwanamke Yule kamchagua kwahiyo anakuwa na hofu ipo siku mtu Yule atakwenda kwa mtu aliekuwa na mvuto zaidi yake au anaependeza zaidi yake, kwahiyo ni vyema ukajikubali na kuto jifananisha na wengine.
- Jiandae Kuishi Maisha Bila Mpenzi Wako
Ndio, najua inaonekana kama ujinga hivi ila sio ukiwa na wivu mara nyingi kitu kinachokuja kichwani ni uoga na unawaza utaishi vipi bila ya mtu Yule, sasa ni vizuri ukawa huru sababu siku akiondoka mtu Yule unaweza changanyikiwa,
Wivu unaondoa mapenzi na unaleta chuki hasira, na mapenzi yanahitaji zaidi uhuru wa nafsi usiwe na uoga wa kumpoteza mtu Yule kwa sababu tu unahisi akiondoka utakufa, jiandae kisaikologia hii itakusaidia kuishi kwa amani kwani hutokuwa na wasiwasi na itapunguza wivu.
- Usimfanyie Mtu Makusudi
Kuna wakati watu wanafanya michezo na mioyo ya watu kumtia mtu wivu makusudi ili aone atafanyaje, usicheze hiyo michezo hii inaonyesha hujiamini kwa mpenzi wako au kwasababu umeona anaongea na mtu na haujapenda sio lazima na wewe umtie wivu siku nyingine na mtu mwingine.
- Acha Kuwaza Vitu ambavyo Havipo
Tunaita “Imagination” watu huwaza sana na kupata picha zao wenyewe kichwani ambazo zinaleta hofu au hata kusababisha kuto kumuamini mtu kabisa, sababu tu unawaza vitu sivyo na ukasababisha matatizo lakini badala yake unaweza tumia mawazo yako kuwaza vitu chanya juu ya mapenzi yenu na usiingie katika matatizo.
- Rabiadamary (mmasaimfupi)
ConversionConversion EmoticonEmoticon