Phiri ameonyesha nia ya kuinasa saini ya beki wa Azam David Mwantika ambaye amekuwa akisota benchi kwa muda mrefu
Kocha Kinnah Phiri ameonyesha nia ya kuinasa saini ya beki wa Azam David Mwantika ambaye amekuwa akisota benchi kwa muda mrefu tangu asajiliwe akitokea Tanzania Prisons.
Kocha Phiri ameiambia Goal, anataka kufanya biashara na Azam kwa kumchukua beki huyo ambaye anaamini anauwezo mkubwa wa kuzuia na hiyo ni baada ya kuwa katika wakati mzuri wa kupata saini ya mshambuliaji Didier Kavumbagu.
“Tunataka kuimarisha kikosi chetu kuziba mapungufu tuliyokuwa nayo msimu uliopita lengo letu ni kuwa na kikosi bora msimu ujao ambacho kitashinda kila taji tutakalo shiriki,”amesema Phiri.
Mwantika ilibaki kidogo asajiliwe Mwadui FC katika usajili wa msimu uliopita lakini urejeo wa kocha Stewart Hall ukambakiza mlinzi huyo ‘aliyejengeka’ katika timu ya Azam kwa mwaka mmoja zaidi ambako amefanikiwa kucheza zaidi ya game 20 katika michuano yote.
Phiri pia anapanga mipango ya kumrejesha mshambuliaji Paul Nonga, ambaye ameomba kuondoka kwenye klabu ya Yanga baada ya kukosa nafasi ya kucheza ikiwa ametumikia miezi minne tu katika mkataba wake wa miaka miwili wa kuichezea Yanga.
-By Zuber Karim Jumaa
ConversionConversion EmoticonEmoticon