Shomari Kapombe kinara Tuzo za msimu Azam

Azam FC ilianza rasmi mchakato wa kusaka mchezaji bora wa timu hiyo kwa msimu uliomalizika hivi karibuni
Klabu ya Azam imetoa tuzo kwa wachezaji wake wanne baada ya kupata kura nyingi kufuatia kutoa mchango mkubwa na kuisaidia timu hiyo kumaliza nafasi ya pili kwenye mashindano ya Ligi ya Vodacom na Kombe la FA.

Mlinzi wa kulia mwenye mabao mengi kwenye ligi ya Vodacom Shomari Kapombe ndiye aliyeibuka kinara kwa kujizolea kura 277, na kipa Aishi Manula akafuatia nafasi ya pili baada ya kupata kura 120 Pascal Wawa raia wa Ivory Coasty akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 40 wakati kiungo mkabaji Himid Mao akishika nafasi ya nne kwa kupata kura 30.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, ameiambia Goal, huo ni utaratibu ambao wamejiwekea kwa lengo la kuwaongezea hamasa ya kujituma wachezaji wao ili kuongeza ushindani na kupata mafanikio.

“Tutatoa zawadi kwa kila mshindi zawadi ambayo itakuwa kubwa lengo na kuamsha ari na kuongeza ushindani kwa wachezaji wetu ili tuweze kufanya vizuri katika mshindano tunayoshiriki,”amesema Kawemba.

Azam FC ilianza rasmi mchakato wa kusaka mchezaji bora wa timu hiyo kwa msimu uliomalizika hivi karibuni ambapo mashabiki wanapata nafasi ya kupiga kura kuchagua mchezaji ambaye wanadhani alitoa mchango mkubwa kwa timu yao.

By Zuber Karim Jumaa
Previous
Next Post »