Moja ya story ambayo imeandikwa June 12 2016 kwenye gazeti la MTANZANIA ni hii yenye kichwa cha habari ‘Ujenzi kiwanja cha ndege Chato wazua nongwa’ Gazeti hilo limeripoti kuwa kusudio la Serikali kujenga kiwanja cha ndege wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita ambako ni nyumbani kwa Rais Dk. John Magufuli limezua mjadala mkubwa.
Gazeti hilo limesema kuwa juzi wakati mbunge wa CHADEMA David Silinde akisoma maoni ya kambi ya Upinzani bungeni, kuhusu hali ya uchumi wa Taifa, Mpango wa Maendeleo ya Taifa na Makadirio ya Mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 pamoja na mambo mengine alihoji juu ya ujenzi huo.
Mtanzania limeripoti kuwa wakati akisoma maoni hayo Silinde alidai tayari uwanja huo umekwishatengewa shilingi bilioni 2 kwa ajili ya upembuzi yakinifu. Kambi hiyo ilihoji kama kuna utafiti wowote ambao Serikali imeufanya na unaonyesha kwamba ujenzi huo unamaslahi na ni kipaumbele cha Taifa kwa sasa.
Aidha Gazeti hilo limesema kuwa kambi hiyo ilishauri Serikali kwanini fedha hizo zilizokwishatengwa zisipelekwe kuimarisha viwanja vilivyopo sasa hasa ikizingatiwa kuwa serikali inataka kununua ndege tatu za shirika Ndege la ATCL.
Kauli hiyo ya Upinzani ndiyo ambayo imezua mijadala hiyo katika mitandao mbalimbali ya kijamii huku baadhi wakimnyooshea kidole moja kwa moja Rais Magufuli juu ya hatua hiyo.
-mtanzania
ConversionConversion EmoticonEmoticon