Matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu wa Yanga 2016 uliofanyika jana June 11 2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam yametangazwa leo June 12 2016, uchaguzi huo ambao matokeo ya awali Yusuph Manji ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti na makamu wake Clement Sanga walionekana kuongoza.
Kwa pamoja Manji na Sanga wamechaguliwa kuiongoza Yanga kwa awamu nyingine tena, Yusuph Manji kashinda kwa jumla ya kura za ndio 1468, hapana 0 na kura zilizoharibika zilikuwa 2, kwa upande wa Sanga ameshinda kwa jumla ya kura 1428 kati ya kura 1508 zilizopigwa huku mpinzani wake Titus Ossoro akipata kura 80 pekee.
- By Rama Mwelondo TZA
ConversionConversion EmoticonEmoticon