Green: Nipo tayari kucheza Simba


Mshambuliaji huyo amewataka Simba kama kweli wanamuhitaji wamfuate kwa mazungumzo na yupo tayari kuwatumikia

Mshambuliaji wa Ndanda FC, Atupele Green amesema yuko tayari kusaini Simba endapo watamfuata.
Kinara huyo wa mabao kwenye michuano ya Kombe la FA, iliyomalizika kwa Yanga kuwa bingwa, ameiambia Goal, pamoja kuwahi kuichezea Yanga lakini hawezi kuiacha ofa ya kucheza Simba kwasababu soka ndiyo ajira yake.
“Siwezi kuchagua timu ya kucheza kwasababu soka ndiyo kazi yangu na ukweli sina mapenzi na timu falani timu yoyote ninayoichezea ndiyo inakuwa yangu,”amesema Atupele.
Mshambuliaji huyo amewataka Simba kama kweli wanamuhitaji wamfuate kwa mazungumzo na yupo tayari kuwatumikia kwani kufanya hivyo anaamini atamfurahisha mama yake mzazi ambaye ni shabiki mkubwa wa Simba.

By Zuber Karim Jumaa
Previous
Next Post »