Yanga waenda kupiga kambi Uturuki kujiandaa kuikabili MO Bejaia

Yanga imezidi kujiimarisha kuelekea michuano ya Kombe la Shirikisho CAF, kuhakikisha wanafanya vizuri dhidi ya Mo Bejaia wameamua kwenda kupiga kambi Uturuki


Yanga inaondoka Jumapili kuelekea Uturuki kupiga kambi ya siku tano kabla ya kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wao wa awali wa kundi A hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mouloudia Olympique Bejaia, ambao utapigwa Juni 19.

Msemaji wa Yanga, Jerry Muro ameiambia Goal, ukiwatoa Juma Abduli na Salum Telela ambao hawatosafiri na timu waliobakia wote wakiwemo wanne wapya watakuwemo kwenye msafara huo kwa ajili ya pambano hilo ambalo wamelipa umuhimu mkubwa kuhakikisha wanashinda.

“Juma Abduli amepatwa na maumivu ya kifundo cha mguu tangu akiwa na timu ya taifa ‘Taifa Stars’ lakini Telela yeye amemaliza mkataba wake na bado hajaongezewa,”amesema Muro.

Kikosi ambacho kitaondoka kuelekea Uturuki makipa ni

Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’, Benedicto Tinocco na Benno Kakolanya.

Mabeki;

Hassan Kessy, Mwinyi Haji, Oscar Joshua, Andrew Vincent ‘Dante’, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Pato Ngonyani na Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro'.

Viungo;


Thabani Kamusoko, Salum Telela, Juma Mahadhi, Said Juma ‘Makapu’, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke na Godfrey Mwashiuya.

Washambuliaji;


Donald Ngoma, Malimi Busungu, Matheo Anthony, Amissi Tambwe na Paul Nonga
.
- By Zuber Karim Jumaa
Previous
Next Post »