Justin Bieber alijikuta akizichapa na pande la mtu usiku wa Jumatano huko Cleveland, Marekani.
Video iliyowekwa na TMZ imemuonesha staa huyo akitoka kwenye hoteli aliyokuwa amefikia na kukutana na mtu aliyeonekana kumrushia ngumi nyepesi. Bieber alicharuka na kuanza kumrushia makonde jamaa huyo kabla ya kuangushwa chini. Watu waliokuwa hapo waliuamua ugomvi huo
Bieber alikuwa mjini humo kwenye mechi ya tatu ya fainali ya NBA kati ya Cleveland Cavaliers na Golden State Warriors.
ConversionConversion EmoticonEmoticon