Majibu ya wabunge wa upinzani kwa Naibu Spika Dk. Tulia baada ya Posho zao kusitishwa



Moja ya story ambayo imeandikwa June 10 2016 kwenye gazeti la Mtanzania ni hii yenye kichwa cha habari ‘Wapinzani wamjibu Naibu Spika Dk Tulia’

Gazeti hilo limeripoti kuwa wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni wamebeza uamuzi uliofanywa na Naibu Spika Dk. Tulia Ackson kwa kusitisha posho zao na kusema hawakwenda Bungeni kufuata malipo hayo.

Kupitia gazeti hilo limenukuu kauli mbalimbali za wabunge wa upinzani wakibeza uamuzi huo wa Naibu Spika, Gazeti hilo limemnukuu David Silinde akisema…….>>> Kauli ya kusitishwa kwa posho za wabunge wa upinzani eti kwa sababu wanatoka kwenye ukumbi wa bunge ni ishara tosha kuwa hajatulia na anakurupuka lakini uamuzi wake huo hautukatishi tamaa wa kuendelea na msimamo wetu dhidi yake’

Gazeti hilo limemnukuu pia Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ……>>> kuhusu hilo suala la posho kwetu sisi si lolote tutaendelea kufanya kazi tuliyotumwa na wananchi kwa kutetea masilahi yao na wala hatukufuata posho’

Gazeti hili pia lilizungumza na Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe ambapo alisema…….>>>Nimeshangazwa na uamuzi na Naibu Spika ndani ya siku tatu kwa jambo moja ametoa uamuzi unaotofautiana, kwanza alieleza kanuni haziruhusu kukatwa posho wabunge jana anasema ameangalia kanuni zinaruhusu iweje mtu mmoja ajipinge mwenyewe’

Previous
Next Post »