Wabunge wa upinzani wametoka nje baada ya Naibu Spika kuingia bungeni


Waziri wa Fedha, Philip Mpango ameingia bungeni na mkoba uliobeba nyaraka za bajeti ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Mpango anamshukuru Rais Magufuli kwa kumteua kuwa waziri wa fedha na anawapongeza wengine waliochaguliwa/kuteuliwa katika nafasi mbalimbali za serikali.

HOTUBA YA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017

Dk. Mpango amesema bajeti imezingatia maoni ya wadau mbalimbali ikiwemo wenye viwanda pia amewashukuru watanzania waliotii Rai ya Rais Magufuli ya kumuombea na kusema bajeti hio ni ya kwanza ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli.

Dk. Mpango amesema bajeti amesema bajeti ina sehemu kuu mbili

  • Kutatua matatizo yanayowakabili wananchi, kufanya mabadiliko makubwa serikalini hususan kuondoa kazi kwa mazoea
  • Kujenga uchumi wa kiwango cha kati kwa uhalisia na kujenga ajira hasa kwa vijana

Dk. Mpango: Kauli mbiu ya bajeti za Afrika Mashariki ni kuongeza uzalishaji viwandani ili kuongeza ajira. Bajeti ya maendeleo imeongezwa mpaka kufikia asilimia 40 kwa mara ya kwanza Tanzania.

Kwa sasa Waziri Mpango anaongolea mapitio ya bajeti ya 2015/16

#Mpango amesema serikali itawasilisha kwa dharula marekebisho ya sheria ya manunuzi ya umma ili manunuzi yaendane na thamani halisi.

Uzalishaji Viwandani
  • Kufikia azma ya viwanda serikali itatekeleza mikakati mbalimbali ikiwemo kulipa fidia kwa ardhi iliyotengwa kwa ajili ya viwanda, kuboresha kupitia viwanda vidogo(SIDO)
  • Serikali itahakikisha viwanda vilivyopo vinafanya kazi ikiwemo
  • Kuchukua hatua stahiki kwa ajili ya wawekezaji wa viwanda walivyobinafsishiwa na serikali.
  • Kuimarisha utoaji wa mikopo kwenye sekta ya viwanda
  • Kuvutia kampuni za nje kuwekeza nchini kwa kuboresha mazingira ya uwekazaji
Utatuzi wa kero za wananchi
  • Rushwa kwenye utoaji wa huduma: Serikali imetenga shilingi 2.5 kuwezesha uanzishwaji wa mahaka za mafisadi.
  • Kutenga pesa kwa ajili ya TAKUKURU ili kutekeleza majukumu yake.
  • Kudhibiti upotevu wa mapato
Wafanyabiashara wanaokaidi kutumia mashine za EFD wanaweza kuzuiwa kufanya biashara nchini kwa miaka 2. Kuanzia July 1 ni marufuku kwa taasisi zote za serikali kufanya biashara na wafanyabiashara wasiotumia mashine za EFD

#Serikali imedhamiria kuondoa kodi kwenye mazao ya kilimo, benki ya kilimo itapanua huduma zake mikoani.

Uchukuzi: Trilioni 2.49 kwa ajili ya upanuzi reli ya kati, ndege mpya na kununua meli na kufanyia ukarabati za zamani. Kuhakikisha TANESCO inakuwa na uwezo kifedha ili lijiendeshe lenyewe.

Elimu: Serikali imetenga trilioni 4.77 sawa na asilimia 22 ya bajeti yote kwa ajili ya elimu ya msingi bila malipo, mikopo elimu ya juu

Maji: Trilioni 1.02 kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa maji ikiwemo ukarabati wa miundombinu ya maji.

Kuboresha mazingira ya kufanya biashara ikiwemo kodi na tozo zinazolalamikiwa, kuboresha huduma za upatikanaji wa mikopo, usambazaji wa gesi asili, kuondoa urasimu na kupambana na rushwa.
  • Serikali imetenga bilioni 2.4 kuboresha makazi ya wazee na watoto
  • Agizo la Rais kupunguza kodi ya mshahara litaanza kutekelezwa Julai mosi
  • Serikali inavipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa nidhamu, utaratibu wa kodi kwenye maduka ya vyombo vya ulinzi utabadilishwa.
Marekebisho kwenye sheria ya kodi
  • Kuondoa kodi kwenye maharage ya soya kwani yalisahauliwa, kuondoa kodi kwenye mbogamboga zote ili kuwezesha upatikanaji wa lishe bora kwa gharama nafuu.
  • Pendekezo la kuondoa kodi kwenye dawa zinazotibu maji.
  • Bidhaa zinazotengezwa Tanzania Bara na kuuzwa Zanzibar zitatozwa VAT na kinyume chake kwani kifungu cha sasa hakina kifungu cha marejesho ya kodi.
  • Kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye bima ya vyombo vya usafiri wa anga kukuza sekta ya Anga na mashirika ya kimataifa kutumia mashirika ya bima ya hapa nchini.
  • Hatua hizi zinatarajiwa kuongeza mapato kwa serikali.
  • Kuondoa msamaha wa kodi kwenye kiinua mgongo cha wabunge kinachotolewa kila baada ya miaka mitano.
Kwa sasa spika anatoa maelezo juu ya miongozo iliyotolewa kuhusu wabunge kususia vikao vya bunge ilhali wanaendelea kulipwa posho.

Naibu spika: Ipo siku tunaweza kujisajili na wote kutoka tabia hii ikiachwa iendelee, bunge liliwahi kutoa muongozo kwa suala kama hili, mwaka 2008 wabunge wa CUF walitoka na kiti na walinyiimwa posho kwa siku zote walizokuwa nje, kitendo cha wabunge kutoka nje ni ukiukwaji wa kanuni.

Wabunge wote wanaojisajili na kutoka nje ya bunge hawatastahili kulipwa posho kwa siku zote ambazo wamekuwa wakijisajili na kutoka nje ya ukumbi wa bunge.

Previous
Next Post »