Wachezaji 10 - Bora katika upachikaji mabao Euro


Zimebaki saa chache kabla ya kuanza michuano ya 15 ya Euro 2016, Romania itashuka dimbani kumenyana na waandazi wa michuano hiyo
Goal inapenda kukupa orodha ya wachezaji 10 waliotikisa kwa kupachika mabao tangu michuano hiyo ilipoanzishwa mwaka 1927
10. Wayne Rooney
Anashikilia rekodi ya ufungaji bora wa muda wote Uingereza. Rooney amecheza michuano ya Euro mwaka 2004, 2012 na mwaka huu pia atakuwepo. Katika awamu mbili zilizopita, amecheza michezo 6 na kufunga magoli matano. Bado yupo katika kinyang’anyiro na pengine ataendelea kufunga mengi zaidi.
9. Savo Milosevic
Mshambulizi huyo wa zamani wa Yugoslavia alicheza mwaka 2000 tu. Alicheza michezo minne na kufunga magoli matano.
8. Nuno Gomez
Nuno Gomez ni nyota wa zamani wa Ureno aliyecheza kwa mafanikio makubwa. Alicheza miaka ya 2000, 2004 na 2008. Alifanikiwa kucheza michezo 14 na kufunga magoli 6.
7. Cristiano Ronaldo
Huyu ni moja ya wachezaji hodari duniani kwa sasa. Ndiye nahodha wa Ureno kwa wakati huu. Amecheza miaka ya 2004, 2008, 2012 na mwaka huu pia atakuwepo. Amefanikiwa kucheza michezo 14 (ukiachana na mwaka huu ambapo bado hajacheza) na kufunga magoli 6.
6. Thierry Henry
Mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa alishiriki michuano hiyo miaka ya 2000, 2004 na 2008. Alifanikiwa kucheza mechi 11 na kuweka kambani magoli 6.
5. Zlatan Ibrahimovic
Nahodha wa Sweden kwa sasa. Ameshiriki michuano hii katika miaka ya 2004, 2008, 2012 na mwaka huu pia yupo. Kabla ya michuano hii ya sasa, amecheza michezo 10 na kufunga magoli 6. Bado ana nafasi ya kujiongezea idadi ya magoli kutokana na uwepo wake katika michuano ya mwaka huu.
4. Patrick Kluivert
Ni moja ya washambuliaji bora wa Uholanzi kuwahi kutokea. Ameshiriki kwenye michuano hiyo katika miaka ya 1996 na 2000. Alicheza michezo 9 na kufunga magoli sita.
3. Ruud van Nistelrooy
Mdachi huyu alikuwa mwiba mchungu kwa safu za ulinzi za timu pinzani. Alishiriki na uholanzi kwenye michuano ya Euro katika miaka ya 2004 na 2008. Alicheza michezo 8 na kufunga magoli 6.
2. Alan Shearer
Shearer ni moja ya washambuliaji bora waliowahi kutokea katika taifa la Uingereza. katika maisha yake yote ya soka ameshiriki michuano ya Euro miaka ya 1992, 1996 na 2000. Alifanikiwa kufunga magoli 7 katika michezo 9.
1. Michel Platini
Licha ya kucheza miaka mingi iliyopita, Platin ambaye ni Mfaransa bado anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi zaidi. Alicheza michuano hiyo mara moja tu, ambapo ilikuwa ni mwaka 1984 na kufunga magoli 9 ndani ya michezo 5.

By Meshack Brighton
Previous
Next Post »